KESHA LA ASUBUHI
Jumatatu 16/4/2018
KUTAFAKARI NENO LA MUNGU
Sheria yako naipenda mno ajabu, ndiyo kutafakari kwangu mchana kutwa. Zaburi 119:97.
Watu hawahitaji ile nuru hafifu ya mila na desturi ili kufanya Maandiko yaeleweke. Ni jambo linaloweza kuonekana kirahisi kama pale mtu anapofikiri kwamba jua, linalong’aa katika mbingu saa sita mchana, linahitaji mwanga hafifu wa kurunzi za duniani kuongeza utukufu wake. Kwenye Biblia, kila wajibu umewekwa wazi, kila fundisho linaeleweka. Karama ya Kristo na mwanga wa Roho Mtakatifu unatufunulia Baba. Neno linao uwezo wa kuwafanya wanaume kwa wanawake na vijana kuwa wenye hekima hadi kufikia wokovu.
“Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema” (2 Timotheo 3:16, 17). Hakuna kitabu kingine chochote chenye nguvu kiasi hicho cha kuweza kuadilisha mawazo, kuongeza nguvu ya akili, kama ukweli unaoadilisha ulio mpana hivyo wa Biblia. Kama Neno la Mungu lingejifunzwa kama ambavyo linastahili, watu wangekuwa na upana wa mawazo, uadilifu wa tabia na kuwa na nia zisizoyumba ambavyo huonekana mara chache nyakati hizi.
Manufaa madogo hupatikana kutokana na usomaji wa haraka wa Maandiko. Mtu anaweza kusoma Biblia yote na bado ashindwe kuona uzuri wake au kuelewa maana yake kwa kina. Sehemu moja inaposomwa mpaka umuhimu wake umekuwa wazi akilini na uhusiano wake na mpango wa wokovu umedhihirika, ina thamani kubwa kuliko kupitia sura nyingi bila kuwa na lengo maalum kichwani na wala kutopata maelekezo thabiti. Kaa na Biblia yako. Ukipata fursa, isome; tunza mafungu akilini mwako. Hata ukitembea mtaani, unaweza kusoma ibara moja na kuitafakari, ukiitunza akilini kwa namna hiyo.
Kamwe usijifunze Biblia bila maombi. Kabla ya kufungua kurasa zake, inatupasa tuombe kuangaziwa na Roho Mtakatifu nasi tutapewa. Nathanieli alipokuja kwa Yesu, Mwokozi alitamka hivi, “Tazama, Mwisraeli kweli kweli, hamna hila ndani yake” (Yohana 1:47). Nathanieli akasema, “Umepataje kunitambua? Yesu akajibu, akamwambia, Kabla Filipo hajakuita, ulipokuwapo chini ya mtini nilikuona” (aya ya 48). Naye Yesu atatuona pia kwenye mahali petu pa siri pa maombi, kama tutamtafuta ili atupatie nuru, ili tupate kujua ukweli ni nini. Malaika wanaotoka kwenye ulimwengu wenye nuru watakuwa pamoja na wale ambao kwa unyenyekevu wa moyo wanatafuta uongozi wa Mungu.
TAFAKARI NJEMA
MAHUSIANO BORA NI JAMBO LA MSINGI KABISA KATIKA MAISHA KATIKA BLOG HII UNAWEZA KUJIFUNZA MENGI SANA KUHUSU MAHUSIANO KATIKA JAMII. KATIBU NA TEMBELEA MARA KWA MARA ILI UWEZE KUNUFAIKA
Monday, 16 April 2018
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Nakuthamini
ikiwa kuna jambo lolote zuri lenye kuboresha au kufundisha usisite kuwasiliana nami. Blog hii ni kwa ajili yetu wote kutufundisha na kutuelekeza yatupasayo kutenda kwa maana wakati umekaribia ambapo yeye ajae anakuja na wala hatakawia. Nyosha mapito yako,tambua tabia yako kila mtafute Bwana maana anapatikana nawe ukimwita atakuitikia.
No comments:
Post a Comment