1.
Maandiko
Matakatifu
Maandiko Matakatifu yaani Agano la Kale na
Jipya ndiyo neno la Mungu lililoandikwa likatolewa kwa uvuvio wa Mungu, kupitia
kwa watu watakatifu wa Mungu walionena na kuandika kama walivyoongozwa na Roho
Mtakatifu. Ndani ya Neno hili, Mungu amemkabidhi mwanadamu maarifa yaliyo
lazima kwa ajili ya wokovu. Maandiko Matakatifu ni ufunuo usioweza kukosa wa
mapenzi yake. Ndiyo upeo wa tabia, kipimo cha uzoefu, ufunuo thabiti wenye
mamlaka wa mafundisho ya imani, na kumbukumbu aminifu ya matendo ya Mungu
katika historia. (IIPet.1:20, 21; IITim. 3:16, 17: Zab. 119:105l Mith. 30:5, 6;
Isa. 8:20; Yoh. 17:17; IWathe. 2:13; Waeb. 4:12)
2.
Utatu
Mtakatifu
Kuna Mungu mmoja: Baba, Mwana, na Roho
Mtakatifu, umoja wa Nafsi tatu za milele. Mungu hapatikani na mauti, mwenye
nguvu zote, ajuaye yote, zaidi ya yote, na aliyeko daima. Yeye hana mwisho na
ni zaidi ya ufahamu wa kibinadamu, hata hivyo anafahamika kupitia kujifunua
kwake Binafsi. Milele zote yu astahili kuabudiwa, kusujudiwa, na viumbe wote.
(Kumb. 6:4; Mathayo 28:19; IIWakor. 13:14; Waef. 4:4-6; IIPet. 1:2; Itim. 1:17;
Ufnl 14:7)
3.
Baba
Mungu Baba wa milele ndiye Muumbaji, chimbuko, Mtegemezaji, na
Mfalme wa viumbe wote. Ni mwenye haki na Mtakatifu, mwingi wa rehema, mwenye
fadhili, si mwepesi wa hsira, ni mwingi wa uthabiti wa upendo na uaminifu.
Tabia na uwezo vilivyodhihirishwa ndani ya Mwana na Roho Mtakatifu pia ni
ufunuo wa Baba. (Mwa. 1:1; Ufun. 4:11; IWakor. 15:28; Yoh. 3:16; IYoh. 4:8;
ITim. 1:17; Kut. 34:6, 7; Yoh. 14:9).
4.
Mwana
Mungu Mwana
wa milele alifanyika mwili katika Yesu Kristo. Kupitia kwake vitu vyote
viliumbwa, tabia ya Mungu imefunuliwa, wokovu wa wanadamu unakamilishwa na
ulimwengu unahukumiwa. Milele zote Mungu kweli, Alifanyika mwanadamu kweli,
Yesu aliye Kristo. Alichukuliwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu na kuzaliwa
na bikira Mariamu. Akaishi na kupitia uzoefu wa majaribu kama mwanadamu, lakini
kwa ukamilifu alionyesha kwa mfano haki na upendo wa Mungu. Kwa miujiza yake
alidhihirisha uwezo wa Mungu na alithibitishwa kama Masihi aliyeahidiwa.
Aliteseka na kufa kwa hiari msalabani kwa ajili ya dhambi zetu, na kuhudumu
katika hekalu la mbinguni kwa niaba yetu. Atakuja tena katika utukufu kwa ajili
ya ukombozi wa mwisho wa watu wake na urejeshwaji wa vitu vyote. (Yoh. 1:1 – 3,
14; Wakol. 1:15 – 19; Yoh. 10:30; Wafil. 2:5 – 11; Waebr. 2:9 – 18; IWakor.
15:3, 4; Waebr. 8:1, 2; Yoh. 14:9; Warumi 6:23: IIWakor. 5:17 – 19; Luka 1:35;
Yoh. 14:1 – 3)
5.
Roho
Mtakatifu
Mungu Roho wa milele alikuwa mtendaji pamoja na Baba na Mwana
katika uumbaji, kufanyika mwili, na katika ukombozi. Aliwavuvia waandishi wa
Maandiko Matakatifu, alijaza maisha ya Kristo na uwezo. Huwavuta na
kuwasadikisha wanadamu; na wale wanaoitikia huwafanya upya na kuwabadilisha
katika sura ya Mungu. Akipelekwa na Baba na Mwana ili kuwa siku zote pamoja na
watoto wake, hutoa karama za kiroho kwa kanisa, huliwezesha kumshuhudia Kristo,
na kwa upatano na Maandiko huliongoza kwenye ukweli wote. (Mwa. 1:2; Luka 1:35;
4:18; Mdo. 10:38; IIPet. 1:21; IIWakor. 3:18; Waef. 4:11, 12; Mdo. 1:8; Yoh.
14:16 – 18, 26; 15:26, 27; 16:7 – 13)
6.
Uumbaji
Mungu ni Muumba wa vitu vyote, na amefunua katika Maandiko
uhalisi wa tukio la shughuli zake za uumbaji. Katika siku sita Bwana alizifanya
“mbingu na nchi” na vitu vyote vilivyo hai juu ya nchi, akastarehe siku ya saba
ya juma lile la kwanza. Na hivyo akaanzisha Sabato kama kumbukumbu ya milele ya
kukamilika kwa kazi yake ya uumbaji. Mwanamume na mwanamke wa kwanza walifanywa
kwa mfano wa Mungu kama upeo wa kazi yake ya uumbaji, wakapewa utawala juu ya
ulimwengu, na wakaagizwa kuwajibika na utunzaji wake. Wakati ulimwengu
ulipomalizika kila kitu kilikuwa “ni chema sana,” ukitangaza utukufu wa Mungu.
(Mwa. 1:2; Kut. 20:8 – 11; Zab. 19:1 – 6; 33:6, 9; Waeb11:3)
7.
Asili
ya Mwanadamu
Mwanamume na Mwanamke walifanywa kwa mfano wa Mungu wakiwa kila
mmoja na nafsi yake, uwezo na uhuru wa kufikiri na kutenda. Ingawa waliumbwa
viumbe huru, kila mmoja ni umoja wa nafsi isiyogawanyika ya mwili, akili na
roho, akimtegemea Mungu kwa uhai na pumzi na mengine yote. Wakati wazazi wetu
wa kwanza walipomwasi Mungu, walikana utegemezi wao kwa Mungu na wakaanguka
kutoka hadhi yao ya juu chini ya Mungu. Sura ya Mungu iliyokuwa ndani yao
iliharibiwa na wakawa chini ya mauti. Wanazaliwa wakiwa na udhaifu na mivuto ya
kuelekea kwenye uovu. Lakini Mungu katika Kristo alipatanisha ulimwengu na
nafsi yake, na kwa njia ya Roho wake hurjesha ndani ya wnadamu watubuo sura ya
Muumba wao. Wakiwa wameumbwa kwa ajili ya utukutu wa Mungu , wanaitwa kumpenda
na kupendana wao wa wao, na kutunza mazingira yao. (Mwa. 1:26 – 28; 2:7; Zab.
8:4 – 8; Mtdo. 17:24 – 28; Mwa. 3; Zab. 51:5; Warumi 5:12 – 17; IIWakor. 5:19,
20; Zab. 51:10; IYoh. 4:7, 8, 11, 20; Mwa. 2:15)
8.
Pambano
Kuu
Jamii yote ya wanadamu sasa inahusika katika pambano kuu baina
ya Kristo na Shetani kuhusu tabia ya Mungu, sheria yake, na utawala wake juu ya
ulimwengu. Ugonvi huu ulianza mbinguni wakati kiumbe aliyeumbwa na kutunukiwa
uhuru wa kuchagua, katika kujiinua akawa shetani, mpinzani wa Mungu, na
kupelekea sehemu ya malaika kwenye uasi. Akaingiza roho ya uasi katika
ulimwengu huu pale alipowaongoza Adamu na Hawa kuingia dhambini. Dhambi hii ya
mwanadamu ilileta matokeo ya upotoshaji wa sura ya Mungu katika wanadamu,
uvurugaji wa ulimwengu ulioumbwa, na mwishowe kuteketea wakati wa gharika
iliyoukumba ulimwengu wote. Ukitazamwa na viumbe wote, ulimwengu huu ukawa
uwanja wa vita ya ulimwengu, ambao kutokana nao Mungu wa upendo hatimaye atathibitika
kuwa mwenye haki. Katika kuwasaidia watu wake katika pambano hili, Kristo
anamtuma Roho Mtakatifu na malaika watiifu kuongoza, kulinda, na kutegemeza
katika njia ya wokovu. (Ufun. 12:4 – 9; Isaya 14: 12 – 14; Ezek. 28:12 – 18;
Mwa. 3; Warumi 1:19 – 32; 5:12 – 21; 8:19 – 22; Mwa. 6 – 8; IIPet. 3:6l IWakor.
4:9; Webr. 1:14)
9.
Maisha,
Mauti na Ufufuo wa Kristo
Katika maisha ya Kristo ya utii mkamilifu kwa mapenzi ya Mungu,
mateso yake, mauti na ufufuo, Mungu alitoa njia pekee ya kafara kwa ajili ya
dhambi ya mwanadamu, ili kwamba wale ambao kwa imani wanapokea upatanisho huu
waweze kuelewa vizuri zaidi upendo mtakatifu usio na kikomo wa Muumbaji. Kafara
hii kamilifu huthibitisha haki ya sheria ya Mungu na fadhili za tabia yake; kwa
sababu hufanya vyote viwili kuhukumu dhambi yetu na kutupatia msamaha. Kifo cha
Kristo ni cha badala na cha kulipia, kupatanisha na chenye kubadilisha. Ufufuo
wa Kristo hutangaza ushindi wa Mungu dhidi ya nguvu za uovu, na kwa wale
wanopokea kafara huhakikisha ushindi wao wa mwisho dhidi ya dhambi na mauti.
Kinatangaza ukuu wa Yesu Kristo, ambaye mbele zake kila goti mbinguni na
duniani litapigwa. (Yoh. 3:16; Isaya 53:1; IPet. 2:21, 22; IWakor. 15:3, 4, 20
– 22; IIWakor. 5:14, 15, 19 – 21; Warumi 1:4; 3:25; 4:25; 8:3, 4; IYoh 2:2;
4:10; Wakol. 2:15; Wafilipi 2: 6 – 11).
10.
Uzoefu
na Wokovu
Katika upendo usio na mwisho na rehema zake Mungu alimfanya
Kristo, asiyejua dhambi kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili kwamba katika yeye
tuweze kufanywa haki ya Mungu. Tukiongozwa na Roho Mtakatifu tunatambua hitaji
letu, tunakiri hali yetu ya kuwa wenye dhambi, tunatubu maasi yetu, na
kuonyesha imani katika Yesu kama Bwana Kristo, kama Mbadala na Kielelezo. Imani
hii inayopokea wokovu huja kupitia katika uwezo wa kimbimgu wa Neno na ni
karama ya neema ya Mungu. Kupitia kwa Kristo tunahesabiwa haki, tunafanywa kuwa
wana na binti za Mungu, na kukombolewa kutoka katika hali ya kuwa chini ya
dhambi. Kupitia kwa Roho tunazaliwa upya na kutakaswa; Roho hufanya upya nia
zetu, huandika sheria ya Mungu ya upendo katika mioyo yetu, na tunapewa uwezo
wa kuishi maisha matakatifu. Tukikaa ndani yake tunakuwa washirika wa asili ya
uungu na tuna hakika ya wokovu sasa na katika hukumu. (IIWakor. 5:17 – 21; Yoh.
3:16; Wag. 1:4; 4:4 – 7; Tito 3:3 – 7; Yoh. 16:8; Wag. 3:13, 14; IPet. 2:21,
22; Warumi 10:17; Luka 17:5; Marko 9:23, 24; Waef. 2:5 – 10; Warumi 3:21 – 26;
Wakol. 1:13, 14; Warumi 8:14 – 17; Wag. 3:26; Yoh. 3:3 – 8; IIPet. 1:3, 4;
Warumi 8:1 – 4; 5:6 – 10)
11.
Kukua
katika Kristo
Kwa kifo chake msalabani Yesu alizishinda nguvu za uovu. Yeye
aliyewatiisha pepo wachafu wakati wa huduma yake hapa duniani amezivunja nguvu
zao na kuthibitisha kuwa mwisho wao ni uangamivu usioepukika. Ushindi wa Yesu
hutupatia ushindi dhidi ya nguvu za uovu ambazo bado zinatafuta kututawala,
tunapotembea naye kwa imani, furaha, na uhakika wa upendo wake. Sasa Roho
Mtakatifu anakaa ndani yetu na kututia nguvu. Tukidumu kujikabidhi kwa Yesu
kama Bwana na Mwokozi wetu tunawekwa huru kutoka katika mzigo wa matendo yetu
yaliyopita. Hatuishi tena gizani, katika hofu ya nguvu za uovu, ujinga, na
katika kukosa maana kwa namna ya maisha yetu ya awali. Katika uhuru huu mpya
ndani ya Kristo, tumeitwa kukua katika kufanana na tabia yake, tukiongea naye
kila siku katika sala, na kujilisha neno lake, tukilitafakari neno lake na
majaaliwa yake, tukiimba sifa zake, tukikusanyika pamoja kwa ajili ya ibada, a
kushiriki katika utume wa kanisa. Tukijitoa katika kuwahudumia kwa upendo wale
wanaotuzunguka na katika kuwashuhudia wokovu wake, kuwepo kwake nasi daima kwa
njia ya Roho hugeuza kila wasaa na kila kazi kuwa uzoefu wa kiroho. (Zab. 1:1,
2; 23:4; 77:11, 12; Kol. 1:13, 14; 2:6, 14, 15; Luka 10:17 – 20; Efeso 5:19,
20; 6:12 – 18; IThes. 5:23; IIPet. 2:9; 3:18; IIWakor. 3:17, 18; Filipi 3:7 –
14; IThes, 5:16 – 18; Math. 20:25 – 28; Yoh. 20:21; Gal. 5:22 – 25; Warumi
8:38, 39; IYoh. 4:4; Waebr. 10:25.)
12.
Kanisa
Kanisa ni jamii ya waumini wanaimkiri Yesu Kristo kuwa Bwana na
Mwokozi wao. Katika kufungamana na watu wa Mungu katika nyakati za Agano la
kale, tunaitwa kutoka katika ulimwengu; na tunajiunga pamoja kwa ajili ya
huduma kwa wanadamu wote, na kwa ajili ya tangazo la injili ulimwenguni mwote.
Kanisa linapata mamlaka yake kutoka kwa Kristo, aliye Neno lililofanyika mwili,
na kutoka katika Maandiko, ambayo ndiyo Neno lililoandikwa. Kanisa ni jamaa ya
Mungu; waliofanywa na Yeye kuwa watoto wake, washiriki wake huishi katika
msingi wa agano jipya. Kanisa ni mwili wa Kristo, jamii ya wale wenye imani
ambayo Kristo mwenyewe ndiye kichwa. Kanisa ni bibi arusi ambaye kwa ajili yake
Kristo alikufa ili apate kulitakasa na kulisafisha. Wakati wa kurudi kwake kwa
ushindi, ataliwasilisha kwake mwenyewe kanisa lenye utukufu, waaminifu wa karne
zote, walionunuliwa kwa damu yake, lisilo na waa au kunyanzi, lakini takatifu
na lisilo na ila. (Mwa. 12:3; Mtdo. 7:38; Waef. 4:11 – 15; 3:8 – 11; Math.
28:19, 20; 16:13 – 20; 18:18; Waef. 2:19 – 22; 1:22, 23; 5:23 – 27 Wakol. 1:17,
18).
13.
Masalio
na Utume Wake
Kanisa la ulimwengu linajumuisha wale wote ambao kwa kweli
wanamwamini Kristo, lakini katika siku za mwisho, kipindi cha kuenea kwa
ukengeufu, masalio wameitwa kuzishika amri za Mungu na imani ya Yesu. Masalio
hawa hutangaza kuwadia kwa saa ya hukumu, hutangaza wokovu kupitia kwa Kristo,
na hupiga mbiu ya kukaribia kwa marejeo yake. Tangazo hili huwakilishwa katika
mfano wa malaika watatu wa ufunuo 14; huambatana na kazi ya hukumu mbinguni na
kuwa na matokeo ya kazi ya toba na matengenezo duniani. Kila muumini anatakiwa
kuwa na sehemu binafsi katika ushuhuda huu wa ulimwenguni kote. (Ufun. 12:17;
14:6 – 12; 18:1 – 4; IIWakor. 5:10; Yuda 1:3, 14; IPet. 1:16 – 19; IIPet. 3:10
– 24; Ufun. 21:1 – 14).
14.
Umoja
katika Mwili wa Kristo
Kanisa ni mwili mmoja ulio na washiriki wengi, walioitwa kutoka
kila taifa, kabila, lugha, na watu. Katika Kristo tu viumbe wapya; ubainishi wa
rangi, tamaduni, elimu, na taifa, na tofauti kati ya tabaka ya juu na ya chini,
tajiri na masikini, mwanamume na mwanamke, havipaswi kuleta mgawanyiko miongoni
mwetu. Sote tu sawa katika Kristo, ambaye kwa Roho mmoja ametufunga katika
ushirika mmoja pamoja na yeye na sisi wenyewe kwa wenyewe; tunapaswa kutumika
na kutumikiwa pasipo upendeleo au kusita. Kupitia kwa ufunuo wa Yesu Kristo
katika Maandiko tunashiriki imani na tumaini moja,, na tunawafikia wote kwa ushuhuda
mmoja. Umoja huu una chimbuko lake katika umoja wa Mungu mmoja mwenye nafsi
tatu ambaye ametufanya sisi kuwa watoto wake. (Warumi 12:4, 5; IWakor. 12:12 –
14; Math. 28:19, 20; Zab. 133:1; IIWakor. 5:16, 17; Mdo. 17:26, 27; Wag. 3:27,
29; Wakol. 3:10 – 15; Waef. 4:14 – 16; 4:1 – 6; Yoh.17:20 – 23)
15.
Ubatizo
Kwa njia ya ubatizo tunakiri imani yetu katika kifo na ufufuo wa
Yesu Kristo, na kushuhudia kufia kwetu dhambi na kusudi letu la kuenenda katika
upya wa maisha. Hivyo tunamkubali Kristo kuwa Bwana na Mwokozi, tunakuwa watu
wake, na tunapokelewa kama washiriki na kanisa lake. Ubatizo ni mfano wa
muungano wetu pamoja na Kristo, msamaha wa dhambi zetu, na kupokea kwetu Roho
mtakatifu. Ni kwa kuzamishwa majini na unategemea uthibitisho wa imani katika
Yesu na ushahidi wa toba ya dhambi. Unafuatia mafunzo katika Maandiko Matakatifu
na ukubali wa mafundisho yake. (Warumi 6:1 – 6; Wakol. 2:1,2,13; Mdo. 16:30 33;
22:16; 2:38; Math. 28:19, 20)
16.
Meza
ya Bwana
Meza ya Bwana ni ushirika katika mfano wa mwili na damu ya Yesu
kama udhihirisho wa imani katika yeye, Bwana na Mwokozi wetu, katika uzoefu huu
wa ushirika Kristo anakuwepo kukutana na kuwaimarisha watu wake. Kadiri
tunavyoshiriki, kwa furaha tunatangaza mauti ya Bwana mpaka arudipo tena.
Maandalizi kwa ajili ya Meza ya Bwana hujumuisha kujihoji nafsi, toba na
ungamo. Bwana aliamuru huduma ya kutawadhana miguu kumaanisha kutakaswa upya,
kuonyesha nia ya kutumikiana wenyewe kwa wenyewe katika unyenyekevu ufananao na
wa Kristo, na kuungana mioyo yetu katika upendo. Huduma ya meza ya Bwana ni
wazi kwa waumini wote Wakristo. (IWakor. 10:16, 17; 11:23 – 30; Math. 26:17 –
30; Ufu. 3:20; Yoh. 6:48 – 63; 13:1 – 17)
17.
Karama
za Roho na Huduma
Mungu huwakirimia washirki wote wa kanisa lake katika kila
kizazi karama za kiroho ambazo kila mshiriki atatumia katika huduma ya upendo
kwa ajili ya mema ya kawaida ya kanisa na ya wanadamu. Zikitolewa kwa wakala wa
Roho Mtakatifu, ambaye humgawia kila mshiriki kama apendavyo yeye, karama hizo
hutoa uwezo wote na huduma zinazohitajiwa na kanisa katika kutekeleza shughuli
zake zilizoamuriwa na Mungu. Kulingana na Maandiko, karama hizi hujumuisha
huduma kama imani, uponyaji, unabii, mahubiri, mafundisho, utawala, upatanisho,
huruma, na huduma ya kujinyima na ufadhili kwa ajili ya msaada na faraja kwa
watu. Baadhi ya washiriki huitwa na Mungu na kukirimiwa na Roho kwa ajili ya
shughuli zinazotambuliwa na kanisa katika uchungaji, uinjilisti, utume, na
huduma za kufundisha zinazohitajika hasa katika kuwapatia zana washiriki kwa
ajili ya huduma, kulijenga kanisa hadi ukomavu wa kiroho, na kukuza umoja wa imani
na maarifa ya Mungu. Pale washiriki wanapozitumia karama hizi za kiroho kama
mawakili waaminifu wa neema mbali mbali za Mungu, kanisa hulindwa dhidi ya
mivuto miharibifu ya mafundisho ya uongo, na hukua kwa ukuaji unaotoka kwa
Mungu, na hujengeka imara katika imani na upendo. (Warumi 12:4 – 8; IWakor.
12:9 – 11, 27, 28; Waef. 4:8, 11 – 16; Mdo 6:1 – 7; ITim. 3:1 – 13; IPet. 4:10,
11.)
18.
Karama
ya Unabii
Mojawapo ya karama za Roho Mtakatifu ni unabii. Karama hii ni
alama – kitambulishi cha kanisa la masalio na ilidhihirishwa katika huduma ya
Ellen G White. Kama mjumbe wa Bwana, maandishi yake ni chanzo kiendelezi na
yenye mamlaka ya ukweli yanayolipatia kanisa faraja, uongozi, mafundisho, na
maonyo. Pia yanaweka wazi kwamba Biblia ndiyo kanuni ambayo kwayo mafundisho
yote na uzoefu lazima vipimwe. (Yoeli 2:28, 29; Mdo. 2:14 – 21; Waebr. 1:1 – 3;
Ufun. 12:17; 19:10)
19.
Sheria
ya Mungu
Kanuni kuu
za sheria ya Mungu zimetiwa pamoja katika amri kumi na mfano wake
ulidhihirishwa katika maisha ya Kristo. Nazo zinadhihirisha upendo wa Mungu,
mapenzi yake, na makusudi yake kuhusu mwenendo wa binadamu na mahusiano nazo ni
sharti kwa watu wote katika kila kizazi. Amri hizi ndiyo msingi wa agano la
Mungu na watu wake na kanuni katika hukumu ya Mungu. Kupitia uwakala wa Roho
Mtakatifu zinasonda dhambi na kuamsha hisia za hitaji la Mwokozi. Wokovu wote
ni katika neema, na si kwa matendo, lakini tunda lake ni utii kwa amri kumi.
Utii huu hukuza upendo wetu kwa Bwana na wajibu kwa ajili ya wanadamu wenzetu.
Utii wa imani hudhihirisha uwezo wa Kristo kubadilisha maisha na hivyo
huimarisha ushuhuda wa Kikristo. (Kut. 20:1 – 17; Zab. 40:7, 8; Math. 22:36 –
40; Kumb. 28:1 – 14; Math. 5:17 – 20; Waebr. 8:8 – 10; Yoh. 15:7 – 10; Waef.
2:8 – 10; IYoh. 5:3; Warumi 8:3, 4; Zab. 19:7 – 14).
20.
Sabato
Muumbaji mkarimu, baada ya siku sita za uumbaji, alipumzika siku
ya saba na kuanzisha Sabato kwa ajili ya watu wote kama kumbukumbu ya uumbaji.
Amri ya nne ya sheria za Mungu zisizobadilika inaagiza adhimisho la Sabato hii
ya siku ya saba kama siku ya mapumziko, ibada, na huduma kulingana na
mafundisho na uzoefu wa Yesu, Bwana wa Sabato. Sabato ni siku ya mawasiliano
yenye furaha pamoja na Mungu na sisi kwa sisi. Ni mfano wa ukombozi wetu katika
Kristo, ishara ya utakaso wetu, ishara ya utii wetu, na mwonjo wa umilele wetu
wa siku zijazo katika ufalme wa Mungu. Sabato ni ishara ya daima ya Mungu ya
agano la milele la Mungu kati yake na watu wake. Utunzaji wa furaha wa wakati
huu mtakatifu toka jioni hadi jioni, jua kuchwa hadi jua kuchwa, ni adhimisho
la matendo ya Mungu ya uumbaji na ukombozi. (Mwa. 2:1 –3; Lut. 20:8 – 11; Luka
4:16; Isaya 56:5, 6; 58:13, 14; Math. 12:1 – 12; Kut. 31:13 – 17; Ezek. 20:12,
20; Kumb. 5:12 – 15; Waebr. 4:1 – 11; Walawi 23:32; Marko 1:32).
21.
Uwakili
Sisi tu mawakili wa Mungu, tuliokabidhiwa na yeye wakati na
fursa, uwezo, na mali, na mibaraka ya dunia na rasilimali zake. Tunawajibika
kwake kwa matumizi yake sahihi. Tunakiri umilikaji wa Mungu kwa huduma ya
uaminifu kwake na kwa wandadmu wenzetu, na kwa kurudisha zaka na kutoa sadaka
kwa ajili ya utangazaji wa injili Yake na kwa utengemezaji na ukuaji wa kanisa
lake. Uwakili ni fursa iliyotolewa kwetu na Mungu kwa ajili ya malezi katika
upendo na ushindi dhidi ya choyo na tamaa. Wakili hufurahia mibaraka inayowajia
wengine kama matokeo ya uaminifu wake. (Mwa. 1:26 – 28; 2:15; INyak 29:14; Hagai
1:3 – 11; Malaki 3:8 – 12; IWakor. 9:9 – 14; Math.23:23; IIWakor. 8:1 – 15;
Warumi 15:26, 27).
22.
Mwenendo
wa Kikristo
Tumeitwa kuwa watauwa wanaofikiri, kujisikia, na kutenda
kulingana na kanuni za mbinguni. Ili Roho aumbe upya ndani yetu tabia ya Bwana
wetu tunajihusisha tu katika mambo yale ambayo yatazaa katika maisha yetu usafi
unaofanana na Kristo, afya na furaha katika maisha yetu. Hii inamaanisha kwamba
maraha na maburudisho yetu yanapaswa kufikia viwango vikuu vya maonji na uzuri
wa Kikristo. Huku tukitambua tofauti za kiutamaduni, mavazi yetu yanapaswa yawe
ya kawaida, si ya anasa; na safi, yanayostahili wale ambao uzuri wao wa kweli
asili yake siyo mapambo ya nje, bali asili yake ni mapambo yasiyoharibika,
yenye roho ya upole na utulivu. Pia inamaanisha kwamba kwa kuwa miili yetu ni
mahekalu ya Roho Mtakatifu, tunapaswa kuitunza kwa akili yenye afya sana kadiri
invyowezekana na kuepuka vyakula vilivyo najisi, vilivyotajwa katika Maandiko
Matakatifu. Kwa vile vinywaji vya vileo, tumbaku na maatumizi mabaya ya madawa
hudhuru miili yetu, yatupasa kuepukana navyo pia. Badala yake tunapaswa
kujishughulisha na cho chote kile kitakacholeta mawazo yetu na miili yetu viwe
katika nidhamu ya Kristo, ambaye hutamani uzima wetu, furaha na wema. (Warumi
12:1, 2; IYoh. 7; 2:6; Waef. 5:1 – 21; Wafilipi 4:8; IIWakor. 10:5; 6:14 – 7:1;
IPet. 3:1 – 4; IWakor. 6:19, 20; 10:31; Walawi 11:1 – 47; IIIYoh. 2).
23.
Ndoa
na Familia
Ndoa ilianzishwa na Mungu katika Edeni na ikathibitishwa na Yesu
kuwa muungano wa maisha yote kati ya mwanamume na mwanamke katika wenzi wenye
upendo. Kwa Mkristo kifungo cha ndoa ni kwa Mungu na pia kwa mwenzi, na
kishirikiwe tu na wenzi wenye imani moja. Upendo wa hiari, heshima, staha, na
uwajibikaji ndizo fito za (kujengea) uhusiano huu, ambao utaakisi upendo,
utakatifu, ukaribu, uthabiti wa uhusiano kati ya Kristo na kanisa lake. Kuhusu
talaka, Yesu alifundisha kwamba mtu anayemwacha mwenzi, isipokuwa kwa sababu ya
uasherati, na akaoa (au kuolewa) na mwingine, azini. Ingawa baadhi ya mahusiano
ya kifamilia huenda yakashindwa kufikia lengo, wenzi katika ndoa ambao
wamejitoa kikamilifu kila mmoja kwa mwenzake katika Kristo wanaweza kufaulu
kufikiliza katika umoja wenye upendo kupitia uongozi wa Roho Mtakatifu na
malezi ya kanisa. Mungu hubariki familia na anakusudia kwamba washirika wake
watasaidiana wao kwa wao kufikia upevu kamili. Wazazi wawalee watoto wao katika
kumpenda na kumtii Bwana. Kwa kielelezo chao na maneno yao wawafundishe kwamba
Kristo ni mtiishaji mwenye upendo, daima mpole na mwenye kujali, anayetaka wawe
viungo vya mwili wake, familia ya Mungu. Kukuza ukaribu wa uhusiano wa
kifamilia ni mojawapo ya alama (ya kujulisha) ujumbe wa mwisho wa injili. (Mwa.
2:18 – 25; Math. 19:3 – 9; Yoh. 2:1 – 11; IIWakor. 6:14; Waef. 5:21 – 33; Math.
5:31, 32; Marko 10:11, 12; Luka 16:18; IWakor. 7:10, 11; Kut. 20:12; Waef. 6:1
– 4; Kumb. 6:5 – 9; Mith. 22:6; Malaki 4:5, 6).
24.
Huduma
ya Kristo katika Hekalu la Mbinguni
Kuna hekalu mbinguni, hema la kweli lililosimamishwa na Bwana na
siyo mwanadamu. Ndani yake Kristo anahudumu kwa niaba yetu, akiwezesha
kupatikana kwa ajili ya waumini fanaka za kafara yake ya upatanisho iliyotolewa
mara moja msalabani kwa ajili ya wote. Alizinduliwa kuwa Kuhani wetu Mkuu na
akaanza huduma yake ya uombezi wakati wa kupaa kwake mbinguni. Mnamo mwaka
1844, mwishoni mwa kipindi cha unabii wa siku 2300, aliingia katika awamu ya
pili na ya mwisho ya huduma yake ya upatanisho. Ni kazi ya hukumu ya upelelezi
ambayo ni sehemu ya mwisho ambayo hatimaye itakomesha dhambi yote, iliyokuwa
mfano wa kutakaswa kwa hekalu la kale la Waebrania katika siku ya upatanisho.
Katika huduma hiyo kielelezo hekalu lilitakaswa kwa damu ya wanyama wa kafara,
lakini mambo ya mbinguni hutakaswa kwa kafara kamili ya damu ya Yesu. Hukumu
ya upelelezi hufunua kwa viumbe wa
mbinguni ni nani miongoni mwa wafu wamelala katika Kristo na hivyo, katika Yeye
wanahesabiwa kustahili kuwa na sehemu katika ufufuo wa kwanza. Pia inadhihirisha
wazi ni nani miongoni mwa walio hai wanakaa ndani ya Kristo, wakishika amri za
Mungu na imani ya Yesu, na katika Yeye, hivyo basi, wako tayari kwa ajili ya
kuhamishwa kuingia katika ufalme wake wa milele. Hukumu hii huthibitisha haki
ya Mungu katika kuwaokoa wale wanaomwamini Yesu. Hutangaza kwamba wale
waliodumu kuwa watiifu kwa Mungu watapokea ufalme. Hitimisho la huduma hii ya
Kristo itakuwa ndiyo mwisho wa kufungwa kwa mlango wa rehema ya wanadamu kabla
ya marejeao ya Yesu. (Waebr.8:1 – 5; 4:14 – 16; 9:11 – 28; 10:19 – 22; 1:3;
2:16, 17; Dan. 7:9 – 27; 8:13, 14; 9:24 – 27; Hes. 14:34; Ezek. 4:6; Walawi 16;
Ufun. 14:6,7; 20:12; 14:12; 22:12).
25.
Kuja
kwa Kristo mara ya pili
Kuja kwa Kristo mara ya pili ndilo tumaini lenye baraka la
kanisa, hitimisho kuu la injili. Kuja kwa Mwokozi kutakuwa halisi, binafsi,
kutakakoonekana, na kwa dunia nzima. Atakaporudi, wenye haki waliokufa
watafufuliwa na pamoja na wenye haki walio hai watavikwa utukufu na kuchukuliwa
kwenda mbinguni, lakini waovu watakufa. Kutimizwa karibu kabisa kwa sehemu
nyingi za unabii pamoja na hali ya sasa ya ulimwengu, huonyesha kwamba kuja kwa
Kristo ku karibu sana. Wakati wa tukio hilo hakukufunuliwa, na hivyo basi
tunahimizwa kuwa tayari kwa nyakati zote. (Tito 2:13; Waebr. 9:28; Yoh. 14:1 –
3; Mdo. 1:9 – 11; Math. 24:14; Ufun. 1:7; Math. 24:43, 44; IWathes. 1: 7 – 10;
2:8; Ufun. 14:14 – 20; 19:11 – 21; Math. 24; Marko 13; Luka 21; IITim. 3:1 – 5;
IWathes. 5:1 – 6).
26.
Mauti
na Ufufuo
Mshahara wa dhambi ni mauti. Lakini Mungu, ambaye peke
yake hapatwi na mauti, atawapa uzima wa milele waliokombolewa wake. Mpaka siku
hiyo mauti ni hali ya kutokuwa na fahamu kwa watu wote. Wakati Kristo, aliye
uzima wetu atakapotokea, wenye haki waliofufuliwa na wenye haki walio hai
watavikwa utukufu na kunyakuliwa juu ili kumlaki Bwana wao. Ufufuo wa pili ni
ufufuo wa waovu, utatokea miaka elfu moja baadaye. (Warumi 6:23; I Tim. 6:15,
15; Mhu. 9:5, 6; Zab. 146:3, 4; Yoh. 11:11 – 14; Wakol. 3:4; IWakor. 15:51 –
54; IWathes. 4:13 – 17; Yoh. 5:28, 29; Ufun. 20:1 – 10)
27.
Milenia
(miaka elfu) na mwisho wa dhambi
Milenia ni
miaka elfu moja ya utawala wa Kristo pamoja na watakatifu wake mbinguni kati ya
ufufuo wa kwanza na wa pili. Wakati huo waovu waliokufa watahukumiwa; dunia
itakuwa ukiwa na utupu bila wanadamu wakazi walio hai, lakini ikikaliwa na
shetani na malaika zake. Mwishowe Kristo na watakatifu wake na Mji Mtakatifu
watashuka duniani kutoka mbinguni. Ndipo waovu waliokufa watafufuliwa, nao
pamoja na shetani na malaika zake watauzingira mji; lakini moto kutoka kwa
Mungu utawateketeza na kuitakasa dunia. Na hivyo ulimwengu utakuwa huru bila
dhambi na wenye dhambi milele. (Ufun. 20; IWakor. 6:2, 3; Yer. 4:23 – 26; Ufun.
21:1 – 5; Malaki 4:1; Ezek. 28:18, 19)
28.
Dunia
mpya
Katika dunia
mpya, ambamo haki hukaa, Mungu ataweka tayari makao ya milele kwa
waliokombolewa na mazingira makamilifu kwa maisha ya milele, upendo, furaha na
kujifunza mbele zake. Kwa kuwa hapa Mungu Mwenyewe atakaa pamoja na watu wake,
na taabu na mauti vitakuwa vimepita. Pambano kuu litakuwa limemalizika, na
dhambi haitakauwako tena. Vitu vyote, vyenye uhai na visivyo na uhai
vitatangaza kwamba Mungu ni pendo; naye atatawala milele. Amina. (IIPet. 3:13;
Isaya 35; 65:17 – 25; Math. 5:5; Ufun. 21:1 – 7; 22:1 – 5; 11:15).
UBARIKIWE MTUMISHI KWA KAZI NZURI
ReplyDelete